Mhubiri 9:16
Ecclesiastes 9:16 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kwa hiyo, nikasema, “Hekima ni bora kuliko nguvu.” Lakini hekima ya maskini imedharauliwa, wala hakuna anayesikiliza maneno yake.
Ecclesiastes 9:16 in English
Ecclesiastes 9:16 · Berean Standard Bible
And I said, “Wisdom is better than strength, but the wisdom of the poor man is despised, and his words are not heeded.”
Context
14Palikuwa na mji mdogo uliokuwa na watu wachache ndani yake. Mfalme mwenye nguvu akainuka dhidi yake, akauzunguka akaweka jeshi kubwa dhidi yake. 15Katika mji huo kulikuwepo mtu mmoja maskini lakini mwenye hekima, naye akauokoa ule mji kwa hekima yake. Lakini hakuna aliyemkumbuka yule maskini. 16Kwa hiyo, nikasema, “Hekima ni bora kuliko nguvu.” Lakini hekima ya maskini imedharauliwa, wala hakuna anayesikiliza maneno yake. 17Maneno ya utulivu ya mwenye hekima
husikiwa kuliko makelele ya mtawala wa wapumbavu. 18Hekima ni bora kuliko silaha za vita,
lakini mwenye dhambi mmoja
huharibu mema mengi.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.