Mhubiri 7:14
Ecclesiastes 7:14 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Nyakati zikiwa nzuri, ufurahi, lakini nyakati zikiwa mbaya, tafakari: Mungu amefanya hiyo moja, naam, sanjari* na hiyo nyingine. Kwa hiyo, mwanadamu hawezi kugundua kitu chochote kuhusu maisha yake ya baadaye.
Ecclesiastes 7:14 in English
Ecclesiastes 7:14 · Berean Standard Bible
In the day of prosperity, be joyful, but in the day of adversity, consider this: God has made one of these along with the other, so that a man cannot discover anything that will come after him.
Context
12Hekima ni ulinzi kama fedha ilivyo ulinzi,
lakini faida ya maarifa ni hii:
kwamba hekima huhifadhi maisha ya aliye nayo. 13Tafakari kile Mungu alichokitenda:
Nani awezaye kunyoosha
kile ambacho yeye amekipinda? 14Nyakati zikiwa nzuri, ufurahi,
lakini nyakati zikiwa mbaya, tafakari:
Mungu amefanya hiyo moja,
naam, sanjari* na hiyo nyingine.
Kwa hiyo, mwanadamu hawezi kugundua
kitu chochote kuhusu maisha yake ya baadaye. 15Katika maisha haya yangu ya ubatili nimeshaona haya mawili:
mtu mwadilifu akiangamia katika uadilifu wake,
naye mtu mwovu akiishi maisha marefu katika uovu wake. 16Usiwe mwenye haki kupita kiasi,
wala usiwe na hekima kupita kiasi:
kwa nini kujiangamiza mwenyewe?
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.