Native Bible

Ecclesiastes 7:12 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Hekima ni ulinzi kama fedha ilivyo ulinzi, lakini faida ya maarifa ni hii: kwamba hekima huhifadhi maisha ya aliye nayo.

Ecclesiastes 7:12 in English

Ecclesiastes 7:12 · Berean Standard Bible

For wisdom, like money, is a shelter, and the advantage of knowledge is that wisdom preserves the life of its owner.

Context

10Usiseme, “Kwa nini siku za kale zilikuwa bora kuliko siku hizi?” Kwa maana si hekima kuuliza maswali kama hayo. 11Hekima, kama ulivyo urithi, ni kitu chema na huwafaidia wale walionalo jua. 12Hekima ni ulinzi kama fedha ilivyo ulinzi, lakini faida ya maarifa ni hii: kwamba hekima huhifadhi maisha ya aliye nayo. 13Tafakari kile Mungu alichokitenda: Nani awezaye kunyoosha kile ambacho yeye amekipinda? 14Nyakati zikiwa nzuri, ufurahi, lakini nyakati zikiwa mbaya, tafakari: Mungu amefanya hiyo moja, naam, sanjari* na hiyo nyingine. Kwa hiyo, mwanadamu hawezi kugundua kitu chochote kuhusu maisha yake ya baadaye.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.