Native Bible

Ecclesiastes 7:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Usiseme, “Kwa nini siku za kale zilikuwa bora kuliko siku hizi?” Kwa maana si hekima kuuliza maswali kama hayo.

Ecclesiastes 7:10 in English

Ecclesiastes 7:10 · Berean Standard Bible

Do not say, “Why were the old days better than these?” For it is unwise of you to ask about this.

Context

8Mwisho wa jambo ni bora kuliko mwanzo wake, uvumilivu ni bora kuliko kiburi. 9Usiwe mwepesi kukasirika rohoni mwako, kwa kuwa hasira hukaa kifuani mwa wapumbavu. 10Usiseme, “Kwa nini siku za kale zilikuwa bora kuliko siku hizi?” Kwa maana si hekima kuuliza maswali kama hayo. 11Hekima, kama ulivyo urithi, ni kitu chema na huwafaidia wale walionalo jua. 12Hekima ni ulinzi kama fedha ilivyo ulinzi, lakini faida ya maarifa ni hii: kwamba hekima huhifadhi maisha ya aliye nayo.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.