Mhubiri 7:15
Ecclesiastes 7:15 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Katika maisha haya yangu ya ubatili nimeshaona haya mawili: mtu mwadilifu akiangamia katika uadilifu wake, naye mtu mwovu akiishi maisha marefu katika uovu wake.
Ecclesiastes 7:15 in English
Ecclesiastes 7:15 · Berean Standard Bible
In my futile life I have seen both of these: A righteous man perishing in his righteousness, and a wicked man living long in his wickedness.
Context
13Tafakari kile Mungu alichokitenda:
Nani awezaye kunyoosha
kile ambacho yeye amekipinda? 14Nyakati zikiwa nzuri, ufurahi,
lakini nyakati zikiwa mbaya, tafakari:
Mungu amefanya hiyo moja,
naam, sanjari* na hiyo nyingine.
Kwa hiyo, mwanadamu hawezi kugundua
kitu chochote kuhusu maisha yake ya baadaye. 15Katika maisha haya yangu ya ubatili nimeshaona haya mawili:
mtu mwadilifu akiangamia katika uadilifu wake,
naye mtu mwovu akiishi maisha marefu katika uovu wake. 16Usiwe mwenye haki kupita kiasi,
wala usiwe na hekima kupita kiasi:
kwa nini kujiangamiza mwenyewe? 17Usiwe mwovu kupita kiasi,
wala usiwe mpumbavu:
kwa nini kufa kabla ya wakati wako?
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.