Mhubiri 5:14
Ecclesiastes 5:14 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
au utajiri uliopotea kwa bahati mbaya, hivyo kwamba wakati akiwa na mwana hakuna chochote kilichobaki kwa ajili yake.
Ecclesiastes 5:14 in English
Ecclesiastes 5:14 · Berean Standard Bible
or wealth lost in a failed venture, so when that man has a son there is nothing to pass on.
Context
12Usingizi wa kibarua ni mtamu,
awe amekula kidogo au kingi,
lakini wingi wa mali
humnyima tajiri usingizi. 13Nimeshaona uovu mzito chini ya jua:
Utajiri uliolimbikizwa kwa kujinyima
na kuleta madhara kwa mwenye mali, 14au utajiri uliopotea kwa bahati mbaya,
hivyo kwamba wakati akiwa na mwana
hakuna chochote kilichobaki kwa ajili yake. 15Mtu hutoka tumboni mwa mama yake uchi,
naye jinsi alivyokuja vivyo hivyo huondoka.
Hachukui chochote kutokana na kazi yake
ambacho anaweza kukibeba mkononi mwake. 16Hili nalo ni baya la kusikitisha:
Kama vile mtu ajavyo, vivyo hivyo huondoka,
naye anapata faida gani,
maadamu hutaabika kwa ajili ya upepo?
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.