Native Bible

Ecclesiastes 4:6 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Afadhali konzi moja pamoja na utulivu kuliko konzi mbili pamoja na taabu na kukimbiza upepo.

Ecclesiastes 4:6 in English

Ecclesiastes 4:6 · Berean Standard Bible

Better one handful with tranquility than two handfuls with toil and pursuit of the wind.

Context

4Tena nikaona kuwa kazi zote na mafanikio yote huchipuka kutokana na wivu wa mtu kwa jirani yake. Hili nalo ni ubatili, ni kukimbiza upepo. 5Mpumbavu hukunja mikono yake na kujiangamiza mwenyewe. 6Afadhali konzi moja pamoja na utulivu kuliko konzi mbili pamoja na taabu na kukimbiza upepo. 7Tena nikaona kitu kingine kilicho ubatili chini ya jua: 8Kulikuwepo mwanadamu aliye peke yake, hakuwa na mwana wala ndugu. Hapakuwa na mwisho wa kazi yake, hata hivyo macho yake hayakutosheka na utajiri wake. Aliuliza, “Ninajitaabisha hivi kwa ajili ya nani, nami kwa nini ninajinyima kufurahia?” Hili pia ni ubatili, ni shughuli yenye taabu!

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.