Native Bible

Ecclesiastes 12:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Maneno ya wenye hekima ni kama mchokoro, mithali zao zilizokusanywa pamoja ni kama misumari iliyogongomewa ikawa imara, yaliyotolewa na Mchungaji mmoja.

Ecclesiastes 12:11 in English

Ecclesiastes 12:11 · Berean Standard Bible

The words of the wise are like goads, and the anthologies of the masters are like firmly embedded nails driven by a single Shepherd.*

Context

9Mhubiri hakuwa tu na hekima, bali aliwagawia watu maarifa pia. Alitafakari na kutafiti na akaweka katika utaratibu mithali nyingi. 10Mhubiri alitafiti ili kupata maneno sahihi na kila alichoandika kilikuwa sawa na kweli. 11Maneno ya wenye hekima ni kama mchokoro, mithali zao zilizokusanywa pamoja ni kama misumari iliyogongomewa ikawa imara, yaliyotolewa na Mchungaji mmoja. 12Tena zaidi ya hayo, mwanangu, kubali maonyo, hakuna mwisho wa kutunga vitabu vingi, nako kusoma sana huuchosha mwili. 13Hii ndiyo jumla ya maneno; yote yamekwisha sikiwa: Mche Mungu, nawe uzishike amri zake, maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.