Mhubiri 12:10
Ecclesiastes 12:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Mhubiri alitafiti ili kupata maneno sahihi na kila alichoandika kilikuwa sawa na kweli.
Ecclesiastes 12:10 in English
Ecclesiastes 12:10 · Berean Standard Bible
The Teacher searched to find delightful sayings and to record accurate words of truth.*
Context
8Mhubiri asema, “Ubatili! Ubatili!
Kila kitu ni ubatili!” 9Mhubiri hakuwa tu na hekima, bali aliwagawia watu maarifa pia. Alitafakari na kutafiti na akaweka katika utaratibu mithali nyingi. 10Mhubiri alitafiti ili kupata maneno sahihi na kila alichoandika kilikuwa sawa na kweli. 11Maneno ya wenye hekima ni kama mchokoro, mithali zao zilizokusanywa pamoja ni kama misumari iliyogongomewa ikawa imara, yaliyotolewa na Mchungaji mmoja. 12Tena zaidi ya hayo, mwanangu, kubali maonyo, hakuna mwisho wa kutunga vitabu vingi, nako kusoma sana huuchosha mwili.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.