Mhubiri 10:5
Ecclesiastes 10:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kuna ubaya niliouona chini ya jua, aina ya kosa litokalo kwa mtawala:
Ecclesiastes 10:5 in English
Ecclesiastes 10:5 · Berean Standard Bible
There is an evil I have seen under the sun— an error that proceeds from the ruler:
Context
3Hata anapotembea barabarani,
mpumbavu hukosa ufahamu
na kudhihirisha kwa kila mmoja
jinsi alivyo mpumbavu. 4Kama hasira ya mtawala ikiwaka dhidi yako,
usiache mahali pako,
utulivu huweza kuzuia makosa mengi. 5Kuna ubaya niliouona chini ya jua,
aina ya kosa litokalo kwa mtawala: 6Wapumbavu kuwekwa kwenye nafasi nyingi za juu,
wakati matajiri hushika nafasi za chini. 7Mimi nimeona watumwa wamepanda farasi,
wakati wakuu wakitembea
kwa miguu kama watumwa.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.