Native Bible

Ecclesiastes 1:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Jua huchomoza na jua huzama, nalo huharakisha kurudi mawioni.

Ecclesiastes 1:5 in English

Ecclesiastes 1:5 · Berean Standard Bible

The sun rises and the sun sets; it hurries back to where it rises.

Context

3Mwanadamu anafaidi nini kutokana na kazi yake yote anayotaabikia chini ya jua? 4Vizazi huja na vizazi hupita, lakini dunia inadumu milele. 5Jua huchomoza na jua huzama, nalo huharakisha kurudi mawioni. 6Upepo huvuma kuelekea kusini na kugeukia kaskazini, hurudia mzunguko huo huo, daima ukirudia njia yake. 7Mito yote hutiririka baharini, hata hivyo bahari kamwe haijai. Mahali mito inapotoka, huko hurudi tena.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.