Native Bible

Deuteronomy 8:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Nguo zenu hazikuchakaa wala miguu yenu haikuvimba kwa miaka hii arobaini.

Deuteronomy 8:4 in English

Deuteronomy 8:4 · Berean Standard Bible

Your clothing did not wear out and your feet did not swell during these forty years.

Context

2Kumbuka jinsi Bwana Mungu wenu alivyowaongoza katika njia yote katika jangwa kwa miaka hii arobaini, kukunyenyekeza na kukujaribu ili ajue lililoko moyoni mwako, kwamba utayashika maagizo yake au la. 3Alikudhili na kukufanya uone njaa kisha akulishe kwa mana, ambayo wewe wala baba zako hamkuijua, awafundishe kuwa mwanadamu hataishi kwa mkate tu bali kwa kila neno litokalo katika kinywa cha Bwana. 4Nguo zenu hazikuchakaa wala miguu yenu haikuvimba kwa miaka hii arobaini. 5Mjue basi ndani ya mioyo yenu kama mtu anavyomwadibisha mwanawe, ndivyo Bwana Mungu wako atawaadibisha ninyi. 6Shikeni maagizo ya Bwana Mungu wenu mtembee katika njia zake na kumheshimu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.