Kumbukumbu 6:12
Deuteronomy 6:12 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
jihadhari usije ukamwacha Bwana, aliyekutoa katika nchi ya Misri, kutoka nchi ya utumwa.
Deuteronomy 6:12 in English
Deuteronomy 6:12 · Berean Standard Bible
be careful not to forget the LORD who brought you out of the land of Egypt, out of the house of slavery.
Context
10Wakati Bwana Mungu wako atakapokuleta katika nchi aliyowaapia baba zako, Abrahamu, Isaki na Yakobo, kukupa wewe, nchi kubwa, ina miji inayopendeza ambayo hukuijenga, 11nyumba zilizojaa vitu vizuri vya aina nyingi ambavyo hukuvijaza, visima ambavyo hukuchimba, na mashamba ya mizabibu na mizeituni ambayo hukupanda wewe, basi, utakapokula na kushiba, 12jihadhari usije ukamwacha Bwana, aliyekutoa katika nchi ya Misri, kutoka nchi ya utumwa. 13Utamcha Bwana Mungu wako, na umtumikie yeye peke yake na kuapa kwa jina lake. 14Usifuate miungu mingine, miungu ya mataifa yanayokuzunguka;
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.