Kumbukumbu 33:20
Deuteronomy 33:20 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kuhusu Gadi akasema: “Atabarikiwa yeye aongezaye milki ya Gadi! Gadi huishi huko kama simba, akirarua kwenye mkono au kichwa.
Deuteronomy 33:20 in English
Deuteronomy 33:20 · Berean Standard Bible
Concerning Gad he said: “Blessed is he who enlarges the domain of Gad! He lies down like a lion and tears off an arm or a head.
Context
18Kuhusu Zabuloni akasema:
“Shangilia, Zabuloni, wakati wa kutoka nje,
nawe Isakari, katika mahema yako. 19Watawaita mataifa kwenye mlima,
na huko mtatoa dhabihu za haki;
watajifurahisha kwa wingi uliojaza bahari,
kwa hazina zilizofichwa mchangani.” 20Kuhusu Gadi akasema:
“Atabarikiwa yeye aongezaye milki ya Gadi!
Gadi huishi huko kama simba,
akirarua kwenye mkono au kichwa. 21Alijichagulia nchi nzuri kuliko zote
kwa ajili yake mwenyewe;
fungu la kiongozi lilikuwa limehifadhiwa
kwa ajili yake.
Viongozi wa watu walipokusanyika,
alitimiza haki ya mapenzi ya Bwana,
na hukumu zake kuhusu Israeli.” 22Kuhusu Dani akasema:
“Dani ni mwana simba,
akiruka kutoka Bashani.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.