Kumbukumbu 33:15
Deuteronomy 33:15 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
pamoja na zawadi bora sana za milima ya zamani na kwa wingi wa baraka za vilima vya milele;
Deuteronomy 33:15 in English
Deuteronomy 33:15 · Berean Standard Bible
with the best of the ancient mountains and the bounty of the everlasting hills,
Context
13Kuhusu Yosefu akasema:
“Bwana na aibariki nchi yake
kwa umande wa thamani
kutoka mbinguni juu,
na vilindi vya maji
vilivyotulia chini; 14pamoja na vitu vilivyo bora sana
viletwavyo na jua,
na vitu vizuri sana vinavyoweza
kutolewa na mwezi; 15pamoja na zawadi bora sana
za milima ya zamani
na kwa wingi wa baraka
za vilima vya milele; 16pamoja na baraka nzuri mno
za ardhi na ukamilifu wake,
na upendeleo wake yeye
aliyeishi kwenye kichaka
kilichokuwa kinawaka moto.
Hivi vyote na vikae juu ya kichwa cha Yosefu,
juu ya paji la uso la aliye mkuu
miongoni mwa ndugu zake. 17Katika fahari yeye ni kama fahali mzaliwa wa kwanza;
pembe zake ni pembe za nyati,
na kwa pembe hizo atapiga mataifa,
hata yaliyo miisho ya dunia.
Hivyo ndivyo yalivyo makumi elfu ya Efraimu;
hivyo ndivyo yalivyo maelfu ya Manase.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.