Kumbukumbu 33:13
Deuteronomy 33:13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Kuhusu Yosefu akasema: “Bwana na aibariki nchi yake kwa umande wa thamani kutoka mbinguni juu, na vilindi vya maji vilivyotulia chini;
Deuteronomy 33:13 in English
Deuteronomy 33:13 · Berean Standard Bible
Concerning Joseph he said: “May his land be blessed by the LORD with the precious dew from heaven above and the deep waters that lie beneath,
Context
11Ee Bwana, bariki ustadi wake wote,
nawe upendezwe na kazi ya mikono yake.
Vipige viuno vya wale wainukao dhidi yake;
wapige adui zake hata wasiinuke tena.” 12Kuhusu Benyamini akasema:
“Mwache mpenzi wa Bwana
apumzike salama kwake,
kwa maana humkinga mchana kutwa,
na yule Bwana ampendaye
hupumzika kati ya mabega yake.” 13Kuhusu Yosefu akasema:
“Bwana na aibariki nchi yake
kwa umande wa thamani
kutoka mbinguni juu,
na vilindi vya maji
vilivyotulia chini; 14pamoja na vitu vilivyo bora sana
viletwavyo na jua,
na vitu vizuri sana vinavyoweza
kutolewa na mwezi; 15pamoja na zawadi bora sana
za milima ya zamani
na kwa wingi wa baraka
za vilima vya milele;
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.