Native Bible

Deuteronomy 32:26 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Nilisema ningewatawanya na kufuta kumbukumbu lao katika mwanadamu.

Deuteronomy 32:26 in English

Deuteronomy 32:26 · Berean Standard Bible

I would have said that I would cut them to pieces and blot out their memory from mankind,

Context

24Nitatuma njaa kali dhidi yao maradhi mabaya, yateketezayo na tauni ya kufisha; nitawapelekea meno makali ya wanyama mwitu, na sumu ya nyoka wale watambaao mavumbini. 25Barabarani upanga utawakosesha watoto; nyumbani mwao hofu itatawala. Vijana wao wa kiume na wa kike wataangamia, pia watoto wachanga na wazee wenye mvi. 26Nilisema ningewatawanya na kufuta kumbukumbu lao katika mwanadamu. 27Lakini nilihofia dhihaka za adui, adui asije akashindwa kuelewa, na kusema, ‘Mikono yetu imeshinda; Bwana hakufanya yote haya.’ ” 28Wao ni taifa lisilo na akili, hakuna busara ndani yao.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.