Native Bible

Deuteronomy 32:17 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Wakatoa dhabihu kwa pepo, ambao si Mungu: miungu wasiyoijua, miungu iliyojitokeza siku za karibuni, miungu ambayo baba zenu hawakuiogopa.

Deuteronomy 32:17 in English

Deuteronomy 32:17 · Berean Standard Bible

They sacrificed to demons, not to God, to gods they had not known, to newly arrived gods, which your fathers did not fear.

Context

15Yeshuruni* alinenepa na kupiga teke; alikuwa na chakula tele, akawa mzito na akapendeza sana. Akamwacha Mungu aliyemuumba, na kumkataa Mwamba Mwokozi wake. 16Wakamfanya Mungu kuwa na wivu kwa miungu yao migeni, na kumkasirisha kwa sanamu zao za machukizo. 17Wakatoa dhabihu kwa pepo, ambao si Mungu: miungu wasiyoijua, miungu iliyojitokeza siku za karibuni, miungu ambayo baba zenu hawakuiogopa. 18Mkamwacha Mwamba, aliyewazaa ninyi; mkamsahau Mungu aliyewazaa. 19Bwana akaona hili, akawakataa, kwa sababu alikasirishwa na wanawe na binti zake.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.