Kumbukumbu 32:15
Deuteronomy 32:15 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Yeshuruni* alinenepa na kupiga teke; alikuwa na chakula tele, akawa mzito na akapendeza sana. Akamwacha Mungu aliyemuumba, na kumkataa Mwamba Mwokozi wake.
Deuteronomy 32:15 in English
Deuteronomy 32:15 · Berean Standard Bible
But Jeshurun * grew fat and kicked— becoming fat, bloated, and gorged. He abandoned the God who made him and scorned the Rock of his salvation.
Context
13Akamfanya apande sehemu zilizoinuka za nchi,
akamlisha kwa mavuno ya mashamba.
Akamlea kwa asali toka mwambani,
na kwa mafuta kutoka mwamba mgumu, 14kwa jibini na maziwa kutoka makundi ya ngʼombe
na kutoka makundi ya mbuzi,
kwa mafuta ya wana-kondoo na mbuzi,
kwa kondoo dume wazuri wa Bashani,
na kwa ngano nzuri.
Ukanywa damu ya zabibu inayotoa povu. 15Yeshuruni* alinenepa na kupiga teke;
alikuwa na chakula tele,
akawa mzito na akapendeza sana.
Akamwacha Mungu aliyemuumba,
na kumkataa Mwamba Mwokozi wake. 16Wakamfanya Mungu kuwa na wivu kwa miungu yao migeni,
na kumkasirisha kwa sanamu zao
za machukizo. 17Wakatoa dhabihu kwa pepo, ambao si Mungu:
miungu wasiyoijua,
miungu iliyojitokeza siku za karibuni,
miungu ambayo baba zenu hawakuiogopa.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.