Kumbukumbu 32:12
Deuteronomy 32:12 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Bwana peke yake alimwongoza; hakuwepo mungu mgeni pamoja naye.
Deuteronomy 32:12 in English
Deuteronomy 32:12 · Berean Standard Bible
The LORD alone led him, and no foreign god was with him.
Context
10Katika nchi ya jangwa alimkuta,
katika nyika tupu ivumayo upepo.
Alimhifadhi na kumtunza;
akamlinda kama mboni ya jicho lake, 11kama tai avurugaye kiota chake,
na kurukaruka juu ya makinda yake,
ambaye hutanda mabawa yake kuwadaka,
na huwachukua kwenye mabawa yake. 12Bwana peke yake alimwongoza;
hakuwepo mungu mgeni pamoja naye. 13Akamfanya apande sehemu zilizoinuka za nchi,
akamlisha kwa mavuno ya mashamba.
Akamlea kwa asali toka mwambani,
na kwa mafuta kutoka mwamba mgumu, 14kwa jibini na maziwa kutoka makundi ya ngʼombe
na kutoka makundi ya mbuzi,
kwa mafuta ya wana-kondoo na mbuzi,
kwa kondoo dume wazuri wa Bashani,
na kwa ngano nzuri.
Ukanywa damu ya zabibu inayotoa povu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.