Kumbukumbu 30:11
Deuteronomy 30:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ninachokuagiza leo sio kigumu sana kwako au usichokiweza.
Deuteronomy 30:11 in English
Deuteronomy 30:11 · Berean Standard Bible
For this commandment I give you today is not too difficult for you or beyond your reach.
Context
9Ndipo Bwana Mungu wako atakapokufanikisha sana katika kazi zote za mikono yako na katika uzao wa tumbo lako, wadogo wa mifugo yako na mazao ya nchi yako. Bwana atakufurahia tena na kukufanikisha, kama alivyowafurahia baba zako, 10kama ukimtii Bwana Mungu wako, na kuzishika amri zake na maagizo yake ambayo yameandikwa katika Kitabu hiki cha Sheria, na kumgeukia Bwana Mungu wako kwa moyo wako wote na kwa roho yako yote. 11Ninachokuagiza leo sio kigumu sana kwako au usichokiweza. 12Hakiko juu mbinguni, ili uulize, “Ni nani atakayepanda mbinguni kukileta na kututangazia ili tuweze kutii?” 13Wala hakiko ngʼambo ya bahari, ili uulize, “Ni nani atakayevuka bahari kwenda kukichukua na kututangazia ili tupate kutii?”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.