Kumbukumbu 3:11
Deuteronomy 3:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
(Mfalme Ogu wa Bashani ndiye peke yake aliyesalia miongoni mwa mabaki ya Warefai. Kitanda chake kilikuwa cha chuma chenye urefu wa dhiraa tisa* na upana wa dhiraa nne.* Mpaka sasa kinaweza kuonekana katika mji wa Waamoni wa Raba.)
Deuteronomy 3:11 in English
Deuteronomy 3:11 · Berean Standard Bible
(For only Og king of Bashan had remained of the remnant of the Rephaim. His bed of iron, nine cubits long and four cubits wide,* is still in Rabbah of the Ammonites.)
Context
9(Wasidoni huuita mlima huo Sirioni, nao Waamori huuita Seniri.) 10Tuliteka miji yote kwenye uwanda wa juu, Gileadi yote, Bashani yote mpaka kufika Saleka na Edrei, miji ya utawala wa Ogu huko Bashani. 11(Mfalme Ogu wa Bashani ndiye peke yake aliyesalia miongoni mwa mabaki ya Warefai. Kitanda chake kilikuwa cha chuma chenye urefu wa dhiraa tisa* na upana wa dhiraa nne.* Mpaka sasa kinaweza kuonekana katika mji wa Waamoni wa Raba.) 12Katika nchi tuliyoiteka wakati ule, niliwapa kabila la Reubeni na Gadi eneo lililoko kaskazini la Aroeri kando ya Bonde la Arnoni, na nusu ya eneo la milima ya Gileadi, pamoja na miji yake. 13Kisha nusu ya kabila la Manase niliwapa sehemu ya Gileadi iliyobaki pamoja na Bashani yote, ambayo ilikuwa utawala wa Ogu. (Eneo lote la Argobu katika Bashani lilikuwa linajulikana kama nchi ya Warefai.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.