Kumbukumbu 3:9
Deuteronomy 3:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
(Wasidoni huuita mlima huo Sirioni, nao Waamori huuita Seniri.)
Deuteronomy 3:9 in English
Deuteronomy 3:9 · Berean Standard Bible
which the Sidonians call Sirion but the Amorites call Senir—
Context
7Lakini wanyama wote wa kufuga pamoja na nyara kutoka kwenye miji yao tulichukua vikawa vyetu. 8Hivyo kwa wakati huo tukachukua kutoka kwa wafalme hawa wawili wa Waamori nchi ya mashariki ya Yordani, kutoka Bonde la Arnoni mpaka kufika kwenye Mlima Hermoni. 9(Wasidoni huuita mlima huo Sirioni, nao Waamori huuita Seniri.) 10Tuliteka miji yote kwenye uwanda wa juu, Gileadi yote, Bashani yote mpaka kufika Saleka na Edrei, miji ya utawala wa Ogu huko Bashani. 11(Mfalme Ogu wa Bashani ndiye peke yake aliyesalia miongoni mwa mabaki ya Warefai. Kitanda chake kilikuwa cha chuma chenye urefu wa dhiraa tisa* na upana wa dhiraa nne.* Mpaka sasa kinaweza kuonekana katika mji wa Waamoni wa Raba.)
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.