Kumbukumbu 27:15
Deuteronomy 27:15 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Alaaniwe mtu afanyaye sanamu ya kuchonga au mwenye kusubu sanamu, kitu ambacho ni chukizo kwa Bwana, kazi ya mikono ya fundi stadi, na kuisimamisha kwa siri.” Kisha watu wote watasema, “Amen!”
Deuteronomy 27:15 in English
Deuteronomy 27:15 · Berean Standard Bible
‘Cursed is the man who makes a carved idol or molten image—an abomination to the LORD, the work of the hands of a craftsman—and sets it up in secret.’ And let all the people say, ‘Amen!’
Context
13Makabila haya yatasimama juu ya Mlima Ebali kwa kutamka laana: Reubeni, Gadi, Asheri, Zabuloni, Dani na Naftali. 14Nao Walawi watawasomea watu wote wa Israeli kwa sauti kubwa: 15“Alaaniwe mtu afanyaye sanamu ya kuchonga au mwenye kusubu sanamu, kitu ambacho ni chukizo kwa Bwana, kazi ya mikono ya fundi stadi, na kuisimamisha kwa siri.”
Kisha watu wote watasema, “Amen!” 16“Alaaniwe mtu amdharauye baba yake na mama yake.”
Kisha watu wote watasema, “Amen!” 17“Alaaniwe mtu asogezaye jiwe la mpaka wa jirani yake.”
Kisha watu wote watasema, “Amen!”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.