Kumbukumbu 23:22
Deuteronomy 23:22 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Lakini ukijizuia kuweka nadhiri, hutakuwa na hatia.
Deuteronomy 23:22 in English
Deuteronomy 23:22 · Berean Standard Bible
But if you refrain from making a vow, you will not be guilty of sin.
Context
20Unaweza kumtoza mgeni riba, lakini siyo nduguyo Mwisraeli, ili kwamba Bwana Mungu wako akubariki katika kila kitu unachoweka mkono katika nchi unayoingia kuimiliki. 21Ukiweka nadhiri kwa Bwana Mungu wako, usichelewe kuitimiza, kwa kuwa Bwana Mungu wako atakudai, nawe utakuwa na hatia ya dhambi. 22Lakini ukijizuia kuweka nadhiri, hutakuwa na hatia. 23Chochote kitakachotamkwa kwa midomo yako ni lazima uhakikishe umekifanya, kwa sababu uliweka nadhiri yako kwa hiari mbele za Bwana Mungu wako kwa kinywa chako mwenyewe. 24Kama ukiingia katika shamba la mizabibu la jirani yako, unaweza kula zabibu kadiri utakavyo, lakini usiweke chochote kwenye kikapu chako.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.