Danieli 7:8
Daniel 7:8 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Wakati nilipokuwa ninafikiri kuhusu pembe hizo, mbele yangu kulikuwa na pembe nyingine, ambayo ni ndogo, iliyojitokeza miongoni mwa zile kumi; pembe tatu za mwanzoni zilingʼolewa ili kuipa nafasi hiyo ndogo. Pembe hii ilikuwa na macho kama ya mwanadamu, na mdomo ulionena kwa majivuno.
Daniel 7:8 in English
Daniel 7:8 · Berean Standard Bible
While I was contemplating the horns, suddenly another horn, a little one, came up among them, and three of the first horns were uprooted before it. This horn had eyes like those of a man and a mouth that spoke words of arrogance.
Context
6“Baada ya huyo, nilitazama, na mbele yangu kulikuwa na mnyama mwingine, aliyefanana na chui. Juu ya mgongo wake alikuwa na mabawa manne kama ya ndege. Mnyama huyu alikuwa na vichwa vinne, naye akapewa mamlaka ya kutawala. 7“Baada ya huyo, katika maono yangu usiku nilitazama, na mbele yangu kulikuwa na mnyama wa nne, mwenye kutisha na kuogofya, tena mwenye nguvu nyingi. Alikuwa na meno makubwa ya chuma; akapondaponda na kuangamiza wahanga wake, na kukanyaga chini ya nyayo zake chochote kilichosalia. Alikuwa tofauti na wanyama wote waliotangulia, naye alikuwa na pembe kumi. 8“Wakati nilipokuwa ninafikiri kuhusu pembe hizo, mbele yangu kulikuwa na pembe nyingine, ambayo ni ndogo, iliyojitokeza miongoni mwa zile kumi; pembe tatu za mwanzoni zilingʼolewa ili kuipa nafasi hiyo ndogo. Pembe hii ilikuwa na macho kama ya mwanadamu, na mdomo ulionena kwa majivuno. 9“Nilipoendelea kutazama,
“viti vya enzi vikawekwa,
naye Mzee wa Siku akaketi.
Mavazi yake yalikuwa meupe kama theluji;
nywele za kichwa chake zilikuwa nyeupe kama sufu.
Kiti chake cha enzi kilikuwa kinawaka kwa miali ya moto,
nayo magurudumu yake yote yalikuwa yanawaka moto. 10Mto wa moto ulikuwa unatiririka,
ukipita mbele yake.
Maelfu elfu wakamhudumia;
kumi elfu mara kumi elfu wakasimama mbele zake.
Mahakama ikakaa kuhukumu,
na vitabu vikafunguliwa.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.