Danieli 2:3
Daniel 2:3 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
akawaambia, “Niliota ndoto inayonisumbua, nami nataka nijue maana yake.”
Daniel 2:3 in English
Daniel 2:3 · Berean Standard Bible
he said to them, “I have had a dream, and my spirit is anxious to understand it.”
Context
1Katika mwaka wa pili wa utawala wake, Nebukadneza aliota ndoto. Mawazo yake yakasumbuka na hakuweza kulala. 2Hivyo mfalme akawaita waganga, wasihiri, wachawi na wanajimu ili wamwambie ndoto yake aliyokuwa ameota. Walipoingia ndani na kusimama mbele ya mfalme, 3akawaambia, “Niliota ndoto inayonisumbua, nami nataka nijue maana yake.” 4Ndipo wanajimu wakamjibu mfalme kwa lugha ya Kiaramu,* “Ee mfalme, uishi milele! Waambie watumishi wako hiyo ndoto, nasi tutaifasiri.” 5Mfalme akawajibu wanajimu, “Nimeamua hivi kwa uthabiti: Ikiwa hamtaniambia ndoto yangu ilikuwa ipi na kuifasiri, mtakatwa vipande vipande na nyumba zenu zitafanywa kuwa vifusi.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.