Native Bible

Daniel 2:1 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Katika mwaka wa pili wa utawala wake, Nebukadneza aliota ndoto. Mawazo yake yakasumbuka na hakuweza kulala.

Daniel 2:1 in English

Daniel 2:1 · Berean Standard Bible

In the second year of his reign, Nebuchadnezzar had dreams that troubled his spirit, and sleep escaped him.

Context

1Katika mwaka wa pili wa utawala wake, Nebukadneza aliota ndoto. Mawazo yake yakasumbuka na hakuweza kulala. 2Hivyo mfalme akawaita waganga, wasihiri, wachawi na wanajimu ili wamwambie ndoto yake aliyokuwa ameota. Walipoingia ndani na kusimama mbele ya mfalme, 3akawaambia, “Niliota ndoto inayonisumbua, nami nataka nijue maana yake.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.