Danieli 2:4
Daniel 2:4 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ndipo wanajimu wakamjibu mfalme kwa lugha ya Kiaramu,* “Ee mfalme, uishi milele! Waambie watumishi wako hiyo ndoto, nasi tutaifasiri.”
Daniel 2:4 in English
Daniel 2:4 · Berean Standard Bible
Then the astrologers answered the king in Aramaic,* “O king, may you live forever! Tell your servants the dream, and we will give the interpretation.”
Context
2Hivyo mfalme akawaita waganga, wasihiri, wachawi na wanajimu ili wamwambie ndoto yake aliyokuwa ameota. Walipoingia ndani na kusimama mbele ya mfalme, 3akawaambia, “Niliota ndoto inayonisumbua, nami nataka nijue maana yake.” 4Ndipo wanajimu wakamjibu mfalme kwa lugha ya Kiaramu,* “Ee mfalme, uishi milele! Waambie watumishi wako hiyo ndoto, nasi tutaifasiri.” 5Mfalme akawajibu wanajimu, “Nimeamua hivi kwa uthabiti: Ikiwa hamtaniambia ndoto yangu ilikuwa ipi na kuifasiri, mtakatwa vipande vipande na nyumba zenu zitafanywa kuwa vifusi. 6Lakini mkiniambia ndoto yangu na kuielezea, mtapokea kwangu zawadi, tuzo na heshima kubwa. Basi niambieni ndoto yangu na mnifasirie.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.