Amosi 5:20
Amos 5:20 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Je, siku ya Bwana haitakuwa giza, na si nuru: giza nene, bila mwonzi wa mwanga?
Amos 5:20 in English
Amos 5:20 · Berean Standard Bible
Will not the Day of the LORD be darkness and not light, even gloom with no brightness in it?
Context
18Ole wenu ninyi mnaoitamani
siku ya Bwana!
Kwa nini mnaitamani siku ya Bwana?
Siku hiyo itakuwa giza, si nuru. 19Itakuwa kama vile mtu aliyemkimbia simba
kumbe akakutana na dubu,
kama vile mtu aliyeingia nyumbani mwake
na kuupumzisha mkono wake kwenye ukuta,
kumbe akaumwa na nyoka. 20Je, siku ya Bwana haitakuwa giza, na si nuru:
giza nene, bila mwonzi wa mwanga? 21“Ninachukia, ninazidharau sikukuu zenu za dini;
siwezi kuvumilia makusanyiko yenu. 22Hata ingawa mnaniletea sadaka zenu za kuteketezwa na sadaka za nafaka,
sitazikubali.
Ingawa mnaniletea sadaka nzuri za amani,
sitazitambua.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.