Native Bible

Amos 5:21 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

“Ninachukia, ninazidharau sikukuu zenu za dini; siwezi kuvumilia makusanyiko yenu.

Amos 5:21 in English

Amos 5:21 · Berean Standard Bible

“I hate, I despise your feasts! I cannot stand the stench of your solemn assemblies.

Context

19Itakuwa kama vile mtu aliyemkimbia simba kumbe akakutana na dubu, kama vile mtu aliyeingia nyumbani mwake na kuupumzisha mkono wake kwenye ukuta, kumbe akaumwa na nyoka. 20Je, siku ya Bwana haitakuwa giza, na si nuru: giza nene, bila mwonzi wa mwanga? 21“Ninachukia, ninazidharau sikukuu zenu za dini; siwezi kuvumilia makusanyiko yenu. 22Hata ingawa mnaniletea sadaka zenu za kuteketezwa na sadaka za nafaka, sitazikubali. Ingawa mnaniletea sadaka nzuri za amani, sitazitambua. 23Niondoleeni kelele za nyimbo zenu! Sitasikiliza sauti za vinubi vyenu.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.