Amosi 5:10
Amos 5:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
mnamchukia yule akemeaye mahakamani, na kumdharau yule ambaye husema kweli.
Amos 5:10 in English
Amos 5:10 · Berean Standard Bible
There are those who hate the one who reproves in the gate and despise him who speaks with integrity.
Context
8(yeye ambaye alifanya Kilimia na Orioni,
ambaye hugeuza giza kuwa mapambazuko
na mchana kuwa usiku,
ambaye huyaita maji ya bahari
na kuyamwaga juu ya uso wa nchi:
Bwana ndilo jina lake; 9yeye hufanya maangamizo kwenye ngome
na kufanya mji uliozungushiwa ngome kuwa ukiwa), 10mnamchukia yule akemeaye mahakamani,
na kumdharau yule ambaye husema kweli. 11Mnamgandamiza maskini
na kumlazimisha awape nafaka.
Kwa hiyo, ingawa mmejenga majumba ya mawe ya fahari,
hamtaishi ndani yake;
ingawa mmepanda mashamba mazuri ya mizabibu,
hamtakunywa divai yake. 12Kwa kuwa ninajua hesabu ya makosa yenu
na ukubwa wa dhambi zenu.
Mmewaonea wenye haki na kupokea rushwa
na kuzuia haki ya maskini mahakamani.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.