Native Bible

Amos 1:13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Hili ndilo asemalo Bwana: “Kwa dhambi tatu za Amoni, hata kwa dhambi nne, sitaizuia ghadhabu yangu. Kwa sababu aliwatumbua wanawake wajawazito wa Gileadi ili kuongeza mipaka yake.

Amos 1:13 in English

Amos 1:13 · Berean Standard Bible

This is what the LORD says: “For three transgressions of the Ammonites, even four, I will not revoke My judgment, because they ripped open the pregnant women of Gilead in order to enlarge their territory.

Context

11Hili ndilo Bwana asemalo: “Kwa dhambi tatu za Edomu, hata kwa dhambi nne, sitaizuia ghadhabu yangu. Kwa sababu alimfuatia ndugu yake kwa upanga, alikataa kuonyesha huruma yoyote, kwa sababu hasira yake kali iliendelea kupanda wakati wote na ghadhabu iliwaka bila kuzuiliwa. 12Nitatuma moto juu ya Temani ambao utateketeza ngome za Bosra.” 13Hili ndilo asemalo Bwana: “Kwa dhambi tatu za Amoni, hata kwa dhambi nne, sitaizuia ghadhabu yangu. Kwa sababu aliwatumbua wanawake wajawazito wa Gileadi ili kuongeza mipaka yake. 14Nitatuma moto kwenye kuta za Raba ambao utateketeza ngome zake katikati ya vilio vya vita katika siku ya mapigano, katikati ya upepo mkali katika siku ya dhoruba. 15Mfalme wake atakwenda uhamishoni, yeye pamoja na maafisa wake,” asema Bwana.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.