Amosi 1:10
Amos 1:10 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Nitatuma moto kwenye kuta za Tiro ambao utateketeza ngome zake.”
Amos 1:10 in English
Amos 1:10 · Berean Standard Bible
So I will send fire upon the walls of Tyre to consume its citadels.”
Context
8Nitamwangamiza mfalme wa Ashdodi
na yeye aishikaye fimbo ya utawala katika Ashkeloni.
Nitaugeuza mkono wangu dhidi ya Ekroni,
hadi Mfilisti wa mwisho atakapokufa,”
asema Bwana Mwenyezi. 9Hili ndilo asemalo Bwana:
“Kwa dhambi tatu za Tiro,
hata kwa dhambi nne, sitaizuia ghadhabu yangu.
Kwa sababu ameuza jumuiya nzima ya mateka kwa Edomu,
na kutokujali mapatano ya undugu, 10Nitatuma moto kwenye kuta za Tiro
ambao utateketeza ngome zake.” 11Hili ndilo Bwana asemalo:
“Kwa dhambi tatu za Edomu,
hata kwa dhambi nne, sitaizuia ghadhabu yangu.
Kwa sababu alimfuatia ndugu yake kwa upanga,
alikataa kuonyesha huruma yoyote,
kwa sababu hasira yake kali iliendelea kupanda wakati wote
na ghadhabu iliwaka bila kuzuiliwa. 12Nitatuma moto juu ya Temani
ambao utateketeza ngome za Bosra.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.