Native Bible

Acts 9:36 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Huko Yafa palikuwa na mwanafunzi jina lake Tabitha (ambalo kwa Kiyunani ni Dorkasi*). Huyu alikuwa mkarimu sana, akitenda mema na kuwasaidia maskini.

Acts 9:36 in English

Acts 9:36 · Berean Standard Bible

In Joppa there was a disciple named Tabitha (which is translated as Dorcas),* who was always occupied with works of kindness and charity.

Context

34Petro akamwambia, “Ainea, Yesu Kristo anakuponya, inuka utandike kitanda chako.” Mara Ainea akainuka. 35Watu wote wa Lida na Sharoni walipomwona Ainea akitembea wakamgeukia Bwana. 36Huko Yafa palikuwa na mwanafunzi jina lake Tabitha (ambalo kwa Kiyunani ni Dorkasi*). Huyu alikuwa mkarimu sana, akitenda mema na kuwasaidia maskini. 37Wakati huo akaugua, akafa na wakiisha kuuosha mwili wake wakauweka katika chumba cha ghorofani. 38Kwa kuwa Yafa hapakuwa mbali sana na Lida, wanafunzi waliposikia kwamba Petro yuko huko waliwatuma watu wawili kwake ili kumwomba, “Tafadhali njoo huku pasipo kukawia.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.