Matendo 9:35
Acts 9:35 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Watu wote wa Lida na Sharoni walipomwona Ainea akitembea wakamgeukia Bwana.
Acts 9:35 in English
Acts 9:35 · Berean Standard Bible
and all who lived in Lydda and Sharon saw him and turned to the Lord.
Context
33Huko alimkuta mtu mmoja aitwaye Ainea, ambaye alikuwa amepooza na kwa muda wa miaka minane alikuwa hajaondoka kitandani. 34Petro akamwambia, “Ainea, Yesu Kristo anakuponya, inuka utandike kitanda chako.” Mara Ainea akainuka. 35Watu wote wa Lida na Sharoni walipomwona Ainea akitembea wakamgeukia Bwana. 36Huko Yafa palikuwa na mwanafunzi jina lake Tabitha (ambalo kwa Kiyunani ni Dorkasi*). Huyu alikuwa mkarimu sana, akitenda mema na kuwasaidia maskini. 37Wakati huo akaugua, akafa na wakiisha kuuosha mwili wake wakauweka katika chumba cha ghorofani.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.