Native Bible

Acts 9:37 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Wakati huo akaugua, akafa na wakiisha kuuosha mwili wake wakauweka katika chumba cha ghorofani.

Acts 9:37 in English

Acts 9:37 · Berean Standard Bible

At that time, however, she became sick and died, and her body was washed and placed in an upper room.

Context

35Watu wote wa Lida na Sharoni walipomwona Ainea akitembea wakamgeukia Bwana. 36Huko Yafa palikuwa na mwanafunzi jina lake Tabitha (ambalo kwa Kiyunani ni Dorkasi*). Huyu alikuwa mkarimu sana, akitenda mema na kuwasaidia maskini. 37Wakati huo akaugua, akafa na wakiisha kuuosha mwili wake wakauweka katika chumba cha ghorofani. 38Kwa kuwa Yafa hapakuwa mbali sana na Lida, wanafunzi waliposikia kwamba Petro yuko huko waliwatuma watu wawili kwake ili kumwomba, “Tafadhali njoo huku pasipo kukawia.” 39Kwa hiyo Petro akainuka akaenda nao, naye alipowasili, wakampeleka hadi kwenye chumba cha ghorofani alipokuwa amelazwa. Wajane wengi walisimama karibu naye wakilia na kuonyesha majoho na nguo nyingine ambazo Dorkasi alikuwa amewashonea alipokuwa pamoja nao.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.