Matendo 7:17
Acts 7:17 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
“Lakini wakati ulipokuwa unakaribia wa kutimizwa kwa ile ahadi ambayo Mungu alikuwa amempa Abrahamu, watu wetu walizidi kuongezeka sana huko Misri.
Acts 7:17 in English
Acts 7:17 · Berean Standard Bible
As the time drew near for God to fulfill His promise to Abraham, our people in Egypt increased greatly in number.
Context
15Hivyo Yakobo akaenda Misri ambako yeye na baba zetu walifia. 16Miili yao ilirudishwa Shekemu na kuzikwa katika kaburi ambalo Abrahamu alinunua kutoka kwa wana wa Hamori kwa kiasi fulani cha fedha. 17“Lakini wakati ulipokuwa unakaribia wa kutimizwa kwa ile ahadi ambayo Mungu alikuwa amempa Abrahamu, watu wetu walizidi kuongezeka sana huko Misri. 18Ndipo mfalme mwingine ambaye hakujua lolote kuhusu Yosefu akatawala Misri. 19Huyu mfalme akawatendea watu wetu hila na kuwatesa baba zetu kwa kuwalazimisha wawatupe watoto wao wachanga ili wafe.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.