Matendo 7:18
Acts 7:18 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Ndipo mfalme mwingine ambaye hakujua lolote kuhusu Yosefu akatawala Misri.
Acts 7:18 in English
Acts 7:18 · Berean Standard Bible
Then another king, who knew nothing of Joseph, arose over Egypt.
Context
16Miili yao ilirudishwa Shekemu na kuzikwa katika kaburi ambalo Abrahamu alinunua kutoka kwa wana wa Hamori kwa kiasi fulani cha fedha. 17“Lakini wakati ulipokuwa unakaribia wa kutimizwa kwa ile ahadi ambayo Mungu alikuwa amempa Abrahamu, watu wetu walizidi kuongezeka sana huko Misri. 18Ndipo mfalme mwingine ambaye hakujua lolote kuhusu Yosefu akatawala Misri. 19Huyu mfalme akawatendea watu wetu hila na kuwatesa baba zetu kwa kuwalazimisha wawatupe watoto wao wachanga ili wafe. 20“Wakati huo Mose alizaliwa, naye hakuwa mtoto wa kawaida. Akalelewa nyumbani kwa baba yake kwa muda wa miezi mitatu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.