Native Bible

Acts 7:20 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

“Wakati huo Mose alizaliwa, naye hakuwa mtoto wa kawaida. Akalelewa nyumbani kwa baba yake kwa muda wa miezi mitatu.

Acts 7:20 in English

Acts 7:20 · Berean Standard Bible

At that time Moses was born, and he was beautiful in the sight of God.* For three months he was nurtured in his father’s house.

Context

18Ndipo mfalme mwingine ambaye hakujua lolote kuhusu Yosefu akatawala Misri. 19Huyu mfalme akawatendea watu wetu hila na kuwatesa baba zetu kwa kuwalazimisha wawatupe watoto wao wachanga ili wafe. 20“Wakati huo Mose alizaliwa, naye hakuwa mtoto wa kawaida. Akalelewa nyumbani kwa baba yake kwa muda wa miezi mitatu. 21Waliposhindwa kumficha zaidi, wakamweka nje mtoni na binti Farao akamchukua akamtunza kama mtoto wake mwenyewe. 22Mose akafundishwa hekima yote ya Wamisri, akawa mtu hodari kwa maneno na matendo.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.