Native Bible

Acts 7:22 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Mose akafundishwa hekima yote ya Wamisri, akawa mtu hodari kwa maneno na matendo.

Acts 7:22 in English

Acts 7:22 · Berean Standard Bible

So Moses was educated in all the wisdom of the Egyptians and was powerful in speech and action.

Context

20“Wakati huo Mose alizaliwa, naye hakuwa mtoto wa kawaida. Akalelewa nyumbani kwa baba yake kwa muda wa miezi mitatu. 21Waliposhindwa kumficha zaidi, wakamweka nje mtoni na binti Farao akamchukua akamtunza kama mtoto wake mwenyewe. 22Mose akafundishwa hekima yote ya Wamisri, akawa mtu hodari kwa maneno na matendo. 23“Mose alipokuwa na umri wa miaka arobaini aliamua kuwatembelea ndugu zake Waisraeli. 24Aliona mmoja wao akidhulumiwa na Mmisri, akamtetea yule aliyeonewa, akampiga yule Mmisri akamuua kulipiza kisasi.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.