Matendo 5:6
Acts 5:6 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Vijana wakaja, wakaufunga mwili wake sanda, wakamchukua nje kumzika.
Acts 5:6 in English
Acts 5:6 · Berean Standard Bible
Then the young men stepped forward, wrapped up his body, and carried him out and buried him.
Context
4Je, kabla hujauza hicho kiwanja si kilikuwa mali yako? Hata baada ya kukiuza, fedha ulizopata si zilikuwa kwenye uwezo wako? Kwa nini basi umewaza hila hii moyoni mwako kufanya jambo kama hili? Wewe hukumwambia uongo mwanadamu bali Mungu.” 5Anania aliposikia maneno haya akaanguka chini na kufa. Hofu kuu ikawapata wote waliosikia jambo lililokuwa limetukia. 6Vijana wakaja, wakaufunga mwili wake sanda, wakamchukua nje kumzika. 7Saa tatu baadaye mkewe Anania akaingia, naye hana habari ya mambo yaliyotukia. 8Petro akamuuliza, “Niambie, je, mliuza kiwanja kwa thamani hii?” Akajibu, “Ndiyo, tuliuza kwa thamani hiyo.”
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.