Matendo 5:5
Acts 5:5 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Anania aliposikia maneno haya akaanguka chini na kufa. Hofu kuu ikawapata wote waliosikia jambo lililokuwa limetukia.
Acts 5:5 in English
Acts 5:5 · Berean Standard Bible
On hearing these words, Ananias fell down and died. And great fear came over all who heard what had happened.
Context
3Petro akamuuliza, “Anania, mbona Shetani ameujaza moyo wako ili kumwambia uongo Roho Mtakatifu, ukaficha sehemu ya fedha ulizopata kutokana na kiwanja? 4Je, kabla hujauza hicho kiwanja si kilikuwa mali yako? Hata baada ya kukiuza, fedha ulizopata si zilikuwa kwenye uwezo wako? Kwa nini basi umewaza hila hii moyoni mwako kufanya jambo kama hili? Wewe hukumwambia uongo mwanadamu bali Mungu.” 5Anania aliposikia maneno haya akaanguka chini na kufa. Hofu kuu ikawapata wote waliosikia jambo lililokuwa limetukia. 6Vijana wakaja, wakaufunga mwili wake sanda, wakamchukua nje kumzika. 7Saa tatu baadaye mkewe Anania akaingia, naye hana habari ya mambo yaliyotukia.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.