Matendo 5:14
Acts 5:14 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Hata hivyo, waliomwamini Bwana wakazidi kuongezeka, wanaume na wanawake.
Acts 5:14 in English
Acts 5:14 · Berean Standard Bible
Yet more and more believers were brought to the Lord—large numbers of both men and women.
Context
12Mitume wakafanya ishara nyingi na miujiza miongoni mwa watu. Walioamini wote walikuwa wakikusanyika katika ukumbi wa Solomoni. 13Hakuna mtu mwingine aliyethubutu kuambatana nao ijapokuwa waliheshimiwa sana na watu. 14Hata hivyo, waliomwamini Bwana wakazidi kuongezeka, wanaume na wanawake. 15Hata wakawa wanawaleta wagonjwa na kuwalaza kwenye magodoro na kwenye vitanda barabarani ili yamkini Petro akipita kivuli chake kiwaguse baadhi yao. 16Pia watu wakakusanyika kutoka miji iliyokuwa karibu na Yerusalemu, wakileta wagonjwa na watu walioteswa na pepo wachafu. Hao wote wakaponywa.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.