Native Bible

Acts 26:27 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Mfalme Agripa, je, unaamini manabii? Najua kuwa unaamini.”

Acts 26:27 in English

Acts 26:27 · Berean Standard Bible

King Agrippa, do you believe the prophets? I know you do.”

Context

25Lakini Paulo akajibu, “Mimi sijarukwa na akili, mtukufu sana Festo, bali nanena kweli nikiwa na akili zangu timamu. 26Naam, Mfalme anajua kuhusu mambo haya yote, nami nasema naye kwa uhuru. Kwa sababu nina hakika kwamba hakuna hata mojawapo ya mambo haya asilolijua, kwa kuwa hayakufanyika mafichoni. 27Mfalme Agripa, je, unaamini manabii? Najua kuwa unaamini.” 28Agripa akamwambia Paulo, “Je, unanishawishi kwa haraka namna hii niwe Mkristo?” 29Paulo akasema, “Ikiwa ni kwa haraka au la, namwomba Mungu, si wewe peke yako bali pia wale wote wanaonisikiliza leo, wawe kama mimi nilivyo, kasoro minyororo hii.”

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.