Matendo 26:28
Acts 26:28 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Agripa akamwambia Paulo, “Je, unanishawishi kwa haraka namna hii niwe Mkristo?”
Acts 26:28 in English
Acts 26:28 · Berean Standard Bible
Then Agrippa said to Paul, “Can you persuade me in such a short time to become a Christian?”
Context
26Naam, Mfalme anajua kuhusu mambo haya yote, nami nasema naye kwa uhuru. Kwa sababu nina hakika kwamba hakuna hata mojawapo ya mambo haya asilolijua, kwa kuwa hayakufanyika mafichoni. 27Mfalme Agripa, je, unaamini manabii? Najua kuwa unaamini.” 28Agripa akamwambia Paulo, “Je, unanishawishi kwa haraka namna hii niwe Mkristo?” 29Paulo akasema, “Ikiwa ni kwa haraka au la, namwomba Mungu, si wewe peke yako bali pia wale wote wanaonisikiliza leo, wawe kama mimi nilivyo, kasoro minyororo hii.” 30Baada ya kusema hayo, mfalme akainuka pamoja na mtawala na Bernike na wale waliokuwa wameketi pamoja nao.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.