Native Bible

Acts 24:11 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Unaweza kuhakikisha kwa urahisi kuwa hazijapita zaidi ya siku kumi na mbili tangu nilipopanda kwenda Yerusalemu kuabudu.

Acts 24:11 in English

Acts 24:11 · Berean Standard Bible

You can verify for yourself that no more than twelve days ago I went up to Jerusalem to worship.

Context

9Pia wale Wayahudi wakaunga mkono wakithibitisha kuwa mashtaka yote haya ni kweli. 10Mtawala Feliksi alipompungia Paulo mkono ili ajitetee, yeye akajibu, “Najua kwamba wewe umekuwa hakimu katika taifa hili kwa miaka mingi, hivyo natoa utetezi wangu kwa furaha. 11Unaweza kuhakikisha kwa urahisi kuwa hazijapita zaidi ya siku kumi na mbili tangu nilipopanda kwenda Yerusalemu kuabudu. 12Hawa wanaonishtaki hawakunikuta nikibishana na mtu yeyote Hekaluni au kuchochea umati wa watu katika sinagogi au mahali pengine popote mjini. 13Wala hawawezi kabisa kukuthibitishia mashtaka haya wanayonishtaki kwayo.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.