Native Bible

Acts 24:13 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015

Wala hawawezi kabisa kukuthibitishia mashtaka haya wanayonishtaki kwayo.

Acts 24:13 in English

Acts 24:13 · Berean Standard Bible

Nor can they prove to you any of their charges against me.

Context

11Unaweza kuhakikisha kwa urahisi kuwa hazijapita zaidi ya siku kumi na mbili tangu nilipopanda kwenda Yerusalemu kuabudu. 12Hawa wanaonishtaki hawakunikuta nikibishana na mtu yeyote Hekaluni au kuchochea umati wa watu katika sinagogi au mahali pengine popote mjini. 13Wala hawawezi kabisa kukuthibitishia mashtaka haya wanayonishtaki kwayo. 14Lakini, ninakubali kwamba mimi namwabudu Mungu wa baba zetu, mfuasi wa Njia, ile ambayo wao wanaiita dhehebu. Ninaamini kila kitu kinachokubaliana na Sheria na kile kilichoandikwa katika Manabii, 15nami ninalo tumaini kwa Mungu, ambalo hata wao wenyewe wanalikubali kwamba kutakuwa na ufufuo wa wafu, kwa wenye haki na wasio na haki.

Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.