Matendo 24:9
Acts 24:9 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Pia wale Wayahudi wakaunga mkono wakithibitisha kuwa mashtaka yote haya ni kweli.
Acts 24:9 in English
Acts 24:9 · Berean Standard Bible
The Jews concurred, asserting that these charges were true.
Context
7Lakini jemadari Lisia alitujia na nguvu nyingi, akamwondoa mikononi mwetu, 8akiwaamuru washtaki wake waje mbele yako: ili] kwa kumchunguza wewe mwenyewe unaweza kujua kutoka kwake mambo yote tunayomshtaki kwayo.” 9Pia wale Wayahudi wakaunga mkono wakithibitisha kuwa mashtaka yote haya ni kweli. 10Mtawala Feliksi alipompungia Paulo mkono ili ajitetee, yeye akajibu, “Najua kwamba wewe umekuwa hakimu katika taifa hili kwa miaka mingi, hivyo natoa utetezi wangu kwa furaha. 11Unaweza kuhakikisha kwa urahisi kuwa hazijapita zaidi ya siku kumi na mbili tangu nilipopanda kwenda Yerusalemu kuabudu.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.