Matendo 15:37
Acts 15:37 · Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version 2015
Barnaba alitaka wamchukue Yohana aitwaye Marko waende naye.
Acts 15:37 in English
Acts 15:37 · Berean Standard Bible
Barnabas wanted to take John, also called Mark.
Context
35Lakini Paulo na Barnaba walibaki Antiokia ambako wao pamoja na wengine wengi walifundisha na kuhubiri neno la Bwana. 36Baada ya muda, Paulo akamwambia Barnaba, “Turudi tukawatembelee ndugu katika miji yote tuliyohubiri neno la Bwana tuone jinsi wanavyoendelea.” 37Barnaba alitaka wamchukue Yohana aitwaye Marko waende naye. 38Lakini Paulo aliona si vyema kwa sababu aliwahi kuwaacha walipokuwa huko Pamfilia, hakutaka kuendelea kufanya kazi naye. 39Pakatokea ubishi mkali kati ya Paulo na Barnaba kuhusu jambo hili, hivyo wakagawanyika. Barnaba akamchukua Yohana Marko wakasafiri baharini kwenda Kipro.
Swahili text and audio: Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version™, made available under an open license by Biblica, Inc.